MOVIES NA VICHEKESHO

Ujumbe wa Fred Vunjabei kwa Vijana | Natamani Vijana Waamue Kufanya Biashara

fred_vunjabei Tuongee kidogo; wengi wanapenda kufanya biashara ila wamekata tamaa, Inawezekana uliwahi kujaribu biashara ukafeli fahamu kuwa hilo sio tatizo kabisa, tayari umefaulu mtihani ambao wengi wanafeli ambao ni kuanza “To start” kama haujui wewe ni bora zaidi ya wengi ambao wanashindwa hata kujaribu.

Mwaka 2015 Forbes walifanya utafiti kuhusu kufeli kwa biashara mpya (Start ups) walisema 90% ya biashara mpya huanguka ndani ya miaka mitano, na 20% huanguka ndani ya mwaka wa kwanza. Sababu kuu ni nyingi ikiwa na kutolifahamu soko vizuri hivyo kutokuwa na bidhaa/huduma sahihi, kuchagua biashara inayohitaji mtaji mkubwa kuliko ulionao, usimamizi mbovu, uchaguzi wa eneo n.k

Mfano miaka kadhaa nyuma kabla ya VUNJABEI niliwahi kujaribu biashara ya nguo ilidumu miezi mitatu tu baada ya kufanya partneship na rafiki yangu pale Kinondoni Studio duka dogo lilikuwa pembeni ya Models Collection, biashara ilikuwa mbaya rafiki yangu akauza duka bila kunambia akakimbia, niliamua kufanya biashara zingine ndogo ndogo nikijipanga lakini miaka mitatu baadae nikarudi kwenye nguo nikaanzia Kariakoo nikiwa nakumbuka mwanzo nilikosea wapi.

Ifahamike kuwa kuanguka ni hatua mojawapo ya kuelekea kwenye mafanikio hutakiwi kukata tamaa LAKINI usirudie biashara ya pili au uliyokosea mwanzo bila kufanya mapitio ukajua sababu ilikuwa nini na wapi ili usirudie makosa, endelea kujaribu na kujaribu usikubali kurudi nyuma wanasema funguo inayofungua mlango huwa ni ile unayojaribu ya mwisho.

Natamani vijana wengi waamue kufanya biashara. Unaposema utaanza kesho na hiyo hofu unayoiendekeza unakosea sana ipo siku utajilaumu na kusema kwanini hatukukwambia.

Maneno ya Yenye Ujumbe Mzito Kutoka kwa Fred Vunjabei (Fred Ngajiro) :

> “Usiponiomba Hela Unakuwa Unipendi”

> “Sio kila Pesa Unayoipata unaona Mfuko wa cement, ISHI”.

kwa mastori zaidi Tembelea Website Yetu Mara kwa Mara www.absalomfamily.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *